NINI HATIMA YAKE
Sehemu ya kwanza(01)
0757207494/0622694992 Email:[email protected]
Ni ndani ya Kijiji cha Mulusi huko kasulu nilipo kuwa kidato cha nne
shule Mulusi sec school sikuwa mwenyeji kutokana na kuhamia hukonikiwa kidato cha nne ,hali ya maisha ilikuwa ngumu sana kwani mama aliuza mihogo yakuchoma na karanga za kuchemsha ili tuweze kuendelea namasomo yetu na kukidhi haja za matumbo yetu...
Ni 2000 nilipo hitimu kidato cha nne kila mtu alinitizama mamahakuwa na matumaini kutokana na kutopata mda mzuri wakujisomea kutokana na kusaidia kazi za nyumbani pia kuchota majiya kuuza , ...Ni usiku wakati wa kula Tazani mwanangu mama aliitanikamtazama na kuitika,... Naam mama yang niliitika
Mama akakohoa kidogo kisha akameza funda la mate na kunitizama
kama mtu anaedadisi kitu flani
"mwanangu nina ugonjwa wa ini pia figo sikuhtaji kukwambia mapema mwanangu nilisubiri uhitimu kidato cha nne "Nilimtazama mama kwa majanga kwani anayoyazungumza kwangu ni kama ndoto na sielewi cha kufanya kwani ugonjwa wa ini na figo unaweza kusababisha kifo mara moja mama alikohoa kisha akaendelea kupunguza Tazani mwanangu siku zangu za kuishivha Duniani zinahesabika ninachokuomba watunze sana wadogo zako hakikisha unawaongoza kutenda yaliyo mema. Mama aliweka kituo kisha akanyamaza nakuchukua mfuko mweusi pembeni yake na kutoa picha aliyoitazama na kuanza kulia
mwanangu huyu mtu hapa kwenye hii picha mtafuteni atawasaidia
Ajab mama hukuongea neno la ziada zaidi akilala kwenye mkekawake na kunyoosha miguu na mikono na mwili wake kuwa mkakamavu baada ya kuyafumba mocho taratibu lakini nilivomuitamuita hakuitika tiyari Mama Tazani alikuwa ameaga Dunia kwa ugonjwa wa ini na figo.
Mazishi yalifanyika na kuisha na kila mtu kutawanyika kuelekea sehemu ya makazi yake
Ni baada ya wiki walikuja watu wawili nisiowajua wakaingia ndani ya nyumba na kuanza kuikagua nyumba chumba hadi bila kusema lolote Kisha mmoja wao aliyeonekana kuwa na kipara pia kitambicha wastani na hakuwa mrefefu sana alivaa suruali la kitambaa na shati la mikono nifupi alichukua simu yake na kuanza kuwasiliana na mtu ambaye sikumfahamu Ndio nyumba nimeiona nitakupatia mil 30 wakijadili kisha akakata simu baada ya kukata simu alinigeukia kisha akasema nawapa siku ya leo na kesho muwekeeni nimeondoka kisha akachukua kiasi cha 50elfu akarudishw kwenye meza hiyo mtatumia kama nauli
Sikutaka kukubaliana na jambo kama hili kizembe hivyo nilipinga lakini jamaa akaniangalia kwa macho ya ukali kisha akaichomoa bastola yake kiunoni na kuninyoshea wewe ndo unajifanya mbabe sio
Sikuongea zaidi ya kutetemeka huku nikilengwa na machozi kwani jamaa alionekana hana masihara Ilibidi niombe msamaha na jamaa taratibu akashusha bastola yake chini na kutuamuru kuondoka siku hiyo nao wakaondoka
Kitendo cha kunyoshewa mguu wa bata kiliwaogopesha wadogo zangu waliokuwa wakishuhudia tulio zima na baada ya watu hawa ambao nilizikariri sura zao licha ya kutofahamu majina yao
Baada ya tulio hilo Tazani aliwashika mikono wadogo zake wawili Albert na wa mwisho Vivian ambae ni wa kike na kuwakalisha chini ili kujadili nini cha kufanya na badala yake walimfikisha uamuzi wa kwenda kwa bibi yao bukoba basi asubuhi na mapema Tazani na wadogo zake waliamua kukusanya vitu vyao pamoja na akiba ya pesa waliyokuwanayo wakichanganya na elfu hamsini walizopewa na kuondoka pale kijijini na kuianza safari ya kuelekea Bukoba huku Tazani akiapa kulipa kwa haya yote waliyofanyiwa
Haya sasa hii ni hatari kuliko kwani roho ya kisasi imemuandama kijanaTazani Nini kitaendelea usikose sehemu ya pili wiki kesho